Heshima yako bro!
Kwenye Makala Haya Tunaangazia...
Najua uko hapa kwa sababu kuna kitu kinakusumbua. Umri umesonga, 40 imekaribia au umeivuka. Ile kasi ya ujana imeanza kupungua, mwili unaanza kuleta mambo ambayo hukuwahi kuyaona. Kitambi kinaanza kujitokeza bila idhini, nguvu zile za zamani zinaanza kupotea kimyakimya, na hata kule chumbani, mambo hayako kama zamani, sio?
Usijali, hauko peke yako. Hiki ndicho kinachowakumba wanaume wengi sana wanapofika au kuvuka umri wa miaka 40. Ni kama vile kuna swichi inazimwa ghafla. Metabolism inakuwa slow balaa, homoni zako, hasa ile muhimu ya kiume (testosterone), zinaanza kuporomoka, na ghafla unajikuta unanenepa kirahisi hata kama unakula kama zamani. Ni madhara yatonayo na mafuta mwilini yanayoanza kujionesha waziwazi.
Mabadiliko Halisi Yanayotokea Kwa Mwanaume Baada ya Miaka 40
Hebu tuwe wakweli kidogo hapa, tuachane na porojo. Kufikisha miaka 40+ kwa mwanaume sio jambo dogo kimwili. Kuna mabadiliko halisi yanatokea:
- Metabolism Inapungua Kasi: Mwili wako auchomi mafuta kama ilivyokuwa nyuma. Hii ndio sababu ya hata kama unakula kiasi kilekile ulichokuwa unakula ukiwa na miaka 25, sasa hivi uzito unaongezeka kirahisi, hasa kwenye tumbo. Hili la jinsi ya kupunguza unene kwa siku 7 huwa linakuwa gumu zaidi.
- Homoni Zinayumba: Kiwango cha Testosterone, homoni kuu ya kiume inayohusika na misuli, nguvu, hamu ya tendo la ndoa, na hata mood, huanza kushuka taratibu. Hii inachangia kupotea kwa misuli, kuongezeka kwa mafuta (hasa tumboni), na kupungua kwa “mzuka”.
- Nguvu na Stamina Kupungua: Unajikuta unachoka haraka zaidi kuliko zamani. Kupanda ngazi mbili tatu kunakutoa jasho. Hata ile shughuli ndogo inakuhitaji upumzike.
- Mafuta Yanajikusanya Tumboni (Kitambi): Hili ndilo janga kubwa kwa wengi wetu. Mafuta haya ya tumboni (visceral fat) sio tu yanaharibu mwonekano, bali ni hatari sana kwa afya. Yanahusishwa na magonjwa ya moyo, kisukari aina ya 2, na hata baadhi ya saratani. Kupunguza mafuta mwilini, hasa tumboni, ni muhimu sana.
- Usingizi Unayumba: Kupata usingizi mzuri na mrefu inaweza kuwa changamoto. Na ukosefu wa usingizi unachochea homoni za stress (cortisol), ambazo zinachangia zaidi kuongezeka kwa mafuta tumboni.
- Changamoto za Chumbani: Hapa ndipo wengi wetu tunaumia kimyakimya. Kupungua kwa hamu, ugumu wa kusimamisha au kudumisha uume... Haya yote yanaweza kuathiriwa na mabadiliko ya homoni, mtiririko wa damu, na hata msongo wa mawazo unaotokana na hali ya mwili.
Ukweli mchungu ni huu: Ukiendelea na mtindo uleule wa maisha uliokuwa nao ukiwa kijana, baada ya 40 utajikuta kwenye matatizo makubwa ya kiafya na hata kupoteza “power” yako kama mwanaume. Afya bora sio kitu cha hiari tena, ni LAZIMA.
Lakini Kuna Habari Njema!
Mimi mwenyewe nilipitia kipindi hiki kigumu. Katikati ya mwaka 2022, niliamua kubadilika. Nilichoka kuona mwili unadhoofika, kitambi kinakuwa kama nembo, na kujiona “mnyonge”. Nilitaka kurudisha ule mwili wa kimichezo, wenye nguvu, na muhimu zaidi, kujisikia vizuri na mwenye kujiamini – ndani na nje ya chumba. Nilifanikiwa kufikia lengo langu la kuwa na asilimia ndogo ya mafuta mwilini, na muhimu zaidi, NINADUMISHA hali hiyo sasa!
Leo, sitaki kukupa hadithi za “six-pack in 7 days” au dawa za miujiza. Nataka kukupa UKWELI – zile tabia halisi, za kila siku, ambazo zimenisaidia mimi (na zinaweza kukusaidia WEWE) kudhibiti uzito, kupunguza mafuta mwilini hatari, na kubaki mkali hata baada ya 40. Hizi ni kanuni za afya bora ambazo nimejifunza na kuzitumia.
Msukumo na Tahadhari Muhimu Kabla Hatujazama
Hizi tabia 10 nilizozikusanya sio za kubahatisha. Ni matokeo ya kusoma vitabu vingi (kama Lifespan ya Dr. Sinclair na How Not To Die ya Dr. Greger), kusikiliza podcast za wataalamu (kama Huberman Lab), na kufuatilia watu wanaojua mambo ya afya kweli (kama Tom Bilyeu).
LAKINI, nitoe tahadhari: Kilichonifanyia kazi mimi huenda kisikufanyie kazi wewe kwa 100%. Kwa mfano, wengine wanasifia kufunga (intermittent fasting) kwa masaa marefu au kufanya mazoezi ukiwa umefunga. Kwa wengine, iliwapandishia homoni za stress (cortisol) kupita kiasi, usingizi ukapotea, na wakashindwa kufuata mpango mzuri wa chakula.
Hivyo, chukua hizi kama MIONGOZO. Jaribu, ona kinachokufaa. Lengo langu ni kukupa cheche za mawazo, kukuchochea ujaribu kitu kipya kitakachokusaidia kufikia na kudumisha afya njema na umbo unalolitaka bila kuteseka.
Jambo la Mwisho Ambalo Muhimu Sana: Mimi siku zote nimekuwa mwembamba kiasili. Kwenye kipindi chote cha ujana wangu nilikuwa sikuwahi kuzidi kilo 60. Kimo changu ni sentimeta 165, hivyo nilikuwa nachezea kwenye uzania wangu.
Mambo yalianza kubadilika mwaka 2020 ambapo uzito wangu ulianza kuongezeka kwa kasi wakati huo nikiwa na umri wa miaka 37 hivi. Mnamo 2022 uliongezeka kufikia 93 na hapo taa nyingi nyekundu ziliwaka na ving’ora juu (mengine nayahifadhi kwa wakati mwingine). Leo hii, March 2025 ninapoandika makala haya, nina 60kg. Ilikuwaje? Ni mjumuisho wa mambo mengi… baadhi nimesha yaandika hapa, na makala hii ni sehemu mojawapo ya safari hiyo.
Sasa, tukiweka hayo kando, twende tukaone hizi tabia 10 za moto zilizoniwezesha kudhibiti mafuta mwilini kwa miaka mitatu na kuendelea!
Tabia #1: TEMBEA KILA UWEZAPO – USICHOKE! Weka Lengo na Livuke!
Hii ndio siri namba moja ambayo watu wengi wanaidharau. Kutembea! Ndio, kutembea tu kwa miguu. Unajua umuhimu wa afya bora unajengwa na vitu vidogo kama hivi?
Kutembea ni njia rahisi na yenye nguvu sana ya kupunguza mafuta mwilini na kuyafanya yasirudi tena. Kwanini?
- Inachoma Kalori Kimyakimya: Unatumia nishati bila hata kujiumiza.
- Haiuchoshi Mwili Kama Mazoezi Makali: Tofauti na kukimbia au kuruka kamba, kutembea hakuupi mwili mshtuko mkubwa, hasa kwa sisi tuliofika 40+ ambapo joints zinaanza kulalamika.
- Mara Chache Huongeza Njaa: Tofauti na mazoezi mengine makali ambayo yanaweza kukufanya utamani kula mlima wote, kutembea hakuongezi sana hamu ya kula.
- Inaboresha Mood: Kutembea, hasa nje kwenye hewa safi, kunasaidia kupunguza stress na kuboresha hali ya akili.
- Inaboresha Sukari Kwenye Damu: Muhimu sana kwa kuzuia kisukari na kudhibiti uzito.
Unapopunguza Uzito: Kutembea kunakusaidia kuunda upungufu wa kalori (calorie deficit) – unachoma zaidi ya unavyokula.
Unapodumisha Uzito: Kutembea kunakuruhusu KULA ZAIDI kidogo bila kuongezeka uzito (hii naipenda sana!), huku ukiimarisha afya yako kwa ujumla.
Jinsi Ninavyofanya (Na Unavyoweza Kufanya):
- Ukienda Dukani/Gym (kama sio mbali sana): TEMBEA! Mimi kwangu ni dakika 25 tu, napiga mwendo.
- Mapumziko ya Dakika 5 Kazini/Nyumbani: SIMAMA NA TEMBEA! Hata kama ni kuzunguka sebuleni au koridoni ofisini.
- Kukutana na Marafiki: Pendekeza KUTEMBEA pamoja badala ya kukaa tu sehemu moja. Pigeni story huku mnachoma kalori. Wewe unayesoma makala hii kama unanifahamu personally, unajua jinsi ambavyo ukitaka kuwa na maongezi nami basi yafanyike kuanzia saa 11:00 jioni aidha tukiwa wote njiani tunatembea au kwenye simu lakini nikiwa njia natembea.
- Wakati wa Kupiga Simu: Tembea huku unaongea. Kwangu mimi huu ndo wakati wakati wa kujibu simu au kupiga simu. Kwa unayenifahamu, kama ulikuwa hujui sababu, basi leo ni siku yako.
- Wakati wa Kusoma/Kuangalia Kitu Kwenye Simu: Hii ndio “silaha yangu ya siri”. Badala ya kukaa kitako, natembea huku naangalia video au kusoma makala. Najua inaonekana kichaa kidogo, lakini imenisaidia kufikisha HATUA 10,000 (lengo langu la chini) kila siku, hata siku nikiwa busy sana. Nimejifunza “fundi” wa kusoma/kuangalia huku natembea. Mara nyingi huwa nasikiliza podcast.
Ujumbe Muhimu: Lengo la hatua 10,000 ni zuri, lakini hata hatua 2,000 au 5,000 ni bora kuliko kukaa tu. Anza na unachoweza. Muhimu ni KUJITAHIDI kwa makusudi KUTEMBEA zaidi kila siku. Fanya iwe tabia. Hii itaongeza matumizi yako ya nishati (calorie expenditure) na kuboresha afya njema yako kwa kiasi kikubwa. Usidharau nguvu ya kutembea!
Tabia #2: USIACHE KUPIGA TIZI LA NGUVU (Strength Training) – Ni Msingi wa Uanaume Baada ya 40!
Sikiliza bro, hii sio hiari. Mazoezi ya kuongeza mwili kwa mwanaume, hasa yale ya nguvu (kupiga vyuma, push-ups, bodyweight exercises), ni MUHIMU SANA unapofikisha na kuvuka miaka 40. Binafsi sikuwa mpenzi kabisa wa kufanya mazoezi, pamoja na kwamba rafiki yangu alikuwa ni mmiliki wa gym. Nilikuwa namtembelea tu. Siku hizi? Nafanya anagalau mara mbili kwa wiki.
Kwanini tizi la nguvu?
- Kuzuia Kupotea kwa Misuli (Sarcopenia): Baada ya miaka 30, tunaanza kupoteza misuli taratibu kama hatufanyi kitu. Kufika 40+, kasi inaongezeka. Mazoezi ya nguvu ndio njia pekee ya kupambana na hili.
- Misuli Inachoma Mafuta: Misuli inahitaji kalori nyingi zaidi ili ijiendeshe, hata ukiwa umepumzika. Kuwa na misuli mingi kunamaanisha metabolism yako itakuwa juu, na itakuwa rahisi kupunguza mafuta mwilini na kudumisha uzito.
- Kuongeza Testosterone: Mazoezi ya nguvu, hasa yale yanayohusisha makundi makubwa ya misuli (squats, deadlifts, bench press), yameonyeshwa kusaidia kuongeza kiwango cha testosterone kiasili. Hii ni muhimu sana kwetu wanaume 40+.
- Kuimarisha Mifupa: Mazoezi ya nguvu yanasaidia kuongeza uzito wa mifupa na kuzuia osteoporosis.
- Kuimarisha Nguvu na Utendaji wa Kila Siku: Kuinua vitu, kucheza na watoto, hata kufanya shughuli za kawaida kunakuwa rahisi zaidi ukiwa na nguvu.
- Kuboresha Muonekano: Misuli inakupa umbo la kiume zaidi, hata kama umepungua uzito. Hutaki kuwa “mwembamba-mnyonge” (skinny fat) – unataka kuwa na mwili imara.
Hatari ya Kuacha Mazoezi Baada ya Kufikia Lengo:
Wengi wanafanya kosa hili. Wanapiga tizi kweli kweli, wanapunguza uzito, halafu wanaacha. NINI KINATOKEA?
- Misuli Inapotea: Mwili ukiona huitumii misuli, unaanza kuipunguza ili kuokoa nishati.
- Metabolism Inashuka: Ukipoteza misuli, unachoma kalori chache.
- Mafuta Yanarudi: Kwa kuwa unachoma kalori chache, inakuwa rahisi sana kurudisha yale mafuta uliyoyapoteza kwa jasho. Utajikuta umerudi kulekule ulipotoka, au hata kuwa na asilimia kubwa zaidi ya mafuta kuliko mwanzo, ingawa uzito unaweza kuwa uleule.
Uzoefu Wangu na Ushauri:
Mimi nilianza na mazoezi ya kunyanyua vitu vizito vya kadri nikiwa nyumbani. Baadaye, nilijiunga na gym ili niweze kutumia uzito mkubwa zaidi na kuendelea kupata matokeo. Wengi huanza na gym moja kwa moja. Haijalishi unaanzia wapi – nyumbani au gym. Jambo la msingi ni KUENDELEA. Fanya iwe sehemu ya maisha yako.
Ni lazima kwenda kila siku? Sikushauri.
Mara Ngapi Kwa Wiki?
Wakufunzi wengi wa YouTube wanapendekeza mara 4-5 kwa wiki. Hiyo ni nzuri kama unaweza. Lakini lengo ni UWE ENDELEVU. Mimi binafsi, kufanya mazoezi zaidi ya siku 3 kwa wiki ilikuwa ngumu kuendana nayo kwa muda mrefu kutokana na ratiba zangu. Kwa hiyo, nimebaki na siku 2 kwa wiki, na BADO nimepata matokeo mazuri sana ya kudumisha misuli na kuwa na asilimia ndogo ya mafuta. Mazoezi ni afya, lakini fanya kiasi unachoweza kudumisha maisha yako yote. Bora siku 2-3 za uhakika kila wiki kuliko 5 – 7 wiki hii na 0 wiki ijayo.
Tafuta program nzuri ya mazoezi ya nguvu inayolenga mwili mzima au igawanye kwa sehemu (mfano: Siku 1 – Kifua & Triceps, Siku 2 – Mgongo & Biceps, Siku 3 – Miguu & Mabega). Hakikisha unaongeza uzito au ugumu taratibu (progressive overload) ili kuendelea kuipa misuli changamoto.
Tabia #3: Jaribu “KUFUNGUA DIRISHA LA KULA” kwa Akili (Smart Intermittent Fasting)
Labda umesikia kuhusu Intermittent Fasting (IF) – ile style ya kula ndani ya muda maalum na kufunga kwa masaa mengine. Kuna aina nyingi, maarufu ikiwa 16:8 (kula ndani ya masaa 8, kufunga masaa 16). Watu wengi wanaisifia kwa kupunguza mafuta mwilini na afya bora.
Kwangu mimi hii haikuwahi kuwa shida. Tangu totoni, kula kwangu mimi saa nyingine kulikuwa kwa fimbo. Ujanani wakati najitegemea, ningeweza kumaliza hata siku tatu, nakunywa maji tu. Nilikuwa nafanya hivyo makusudi kama ilivyo sasa? Hapana. Sikuwa naumwa njaa.
Najua kwa wengi wetu, mamabo yanaanzaga kubadilika baada ya kuoa. Kwa mwanamke, yeye kukupa chakula kila wakati uwapo nyumbani.. kwao ni ishara ya upendo na kujali. Na siye ili tuonekane ni romamtic, tunakula.
Baadaye mwili unazoea… kwenye umri wa ujana hii siyo issue. Kwa sababu kiwango cha testosterone kinakuwa juu, vivyo hivyo uunguzwaji wa mafuta unakuwa juu. Huoti kitambi. Vipi, baada ya miaka 40 na mwili ulishauzoesha chakula?
Majibu uko nayo mwenyewe…
Na kama nilivyosema awali, kwa wengine ile 16:8 kali haifanya kazi. Iliwaongezea stress, iliharibu usingizi wao. Baada ya kuacha, usingizi ulirudi.
Lakini…
Bado naamini IF ina faida zake kubwa, hasa katika kudhibiti ulaji. Inakusaidia kuepuka kula hovyo siku nzima.
“IF ya Kistaarabu” (My Approach):
Badala ya kufunga kwa masaa 16, mimi najaribu kufunga kwa masaa 12 hadi 14. Hii ni rahisi zaidi kufanya na haiupi mwili stress kubwa.
- Mfano: Napata kifungua kinywa kati ya saa 3-5 asubuhi, na chakula changu cha mwisho (dinner) kinakuwa karibu saa 2 usiku. Hii inanipa muda wa masaa kama 13-14 ya kutokula (ambayo mengi ni wakati nikiwa nimelala).
- Faida: Hii inanisaidia kuepuka kula usiku sana (tabia mbaya sana ya kuongeza mafuta) na pia inanipa muda wa kutosha wa mmeng’enyo kabla ya kulala, hivyo kulala vizuri zaidi. Pia inapunguza nafasi za kula vitu vidogovidogo (snacks) kati ya milo mikuu.
Kwa Mwanaume 40+:
Kudhibiti stress ni muhimu sana baada ya 40, kwani homoni ya cortisol inapokuwa juu, inachochea sana uhifadhi wa mafuta tumboni. Aina kali za IF zinaweza kuongeza cortisol kwa baadhi ya watu. Hii “IF ya kistaarabu” ya masaa 12-14 inaweza kuwa njia nzuri ya kupata faida za IF (kudhibiti ulaji, kuboresha insulin sensitivity) bila kuongeza stress isiyo ya lazima mwilini wakati huo ukiuandaa mwili kwa ajili ya ile 16:8.
Jaribu kuweka muda wako wa kula uwe kati ya masaa 10 hadi 12 kwa siku. Kwa mfano, kula kati ya saa 1 asubuhi hadi saa 11 jioni, au saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni. Sikiliza mwili wako. Kama unajisikia vizuri, endelea. Kama inakuletea shida (kukosa usingizi, kuishiwa nguvu sana, hasira), basi punguza muda wa kufunga au achana nayo. Kumbuka, lengo ni afya njema endelevu.
Tabia #4: FAHAMU UNACHOKULA – Fuatilia Kalori (Lakini kwa Akili, sio Ukichaa!)
Hapa najua wengi watakunja uso. “Kuhesabu kalori? Aah, kazi gani hiyo?”
Nielewe vizuri. Kuwa obsessed na kuhesabu kila kalori kunaweza kuharibu uhusiano wako na chakula, na hiyo sio nzuri.
LAKINI…
Kuwa na ufahamu wa kiasi gani cha kalori unachokula kunaweza kuwa na nguvu kubwa sana katika safari yako ya kupunguza mafuta mwilini na kudumisha afya bora. Kwangu mimi, ilikuwa game-changer.
Kwanini Kufuatilia (kwa Akili) Kunasaidia:
- Inakupa Udhibiti: Unajua kinachoingia mwilini mwako. Hukubahatishi.
- Inakupa Uhuru wa Kujiruhusu: Ukijua “bajeti” yako ya kalori, unaweza kupanga kujiruhusu kula vitu unavyopenda (kama pizza au bia) mara moja moja bila kuharibu mpango mzima. Unajua jinsi ya kufidia baadaye.
- Inakufundisha Kuhusu Chakula: Unaanza kujua ni vyakula gani vina kalori nyingi bila virutubisho (empty calories) na vipi vina virutubisho vingi kwa kalori chache (nutrient-dense). Hii inakusaidia kufanya chaguzi bora zaidi.
Mbinu Yangu ya “Weekly Average”:
Badala ya kuhangaika kufikia lengo la kalori kila siku moja, mimi naangalia wastani wa WIKI NZIMA.
- Mfano: Tuseme nahitaji kalori 2,000 kwa siku ili kudumisha umbo langu (hii sio namba yangu halisi). Hiyo ni kalori 14,000 kwa wiki.
- Jinsi Inavyofanya Kazi: Kama Ijumaa nikatoka na washkaji na nikapiga kalori 4,000 siku hiyo, SIJILAUMU wala kujiona nimefeli. Najua tu kwamba kwa siku zilizobaki za wiki, nahitaji kupunguza kidogo ili wastani wa wiki ubaki ndani ya 14,000. Labda siku nne zijazo nitakula kalori 1,500 kila siku. Hii inanipa flexibility na kufanya maisha yawe rahisi zaidi kuishi.
Jinsi ya Kuanza:
- Tumia app za simu kama MyFitnessPal au Lose It! kwa wiki chache tu ili kupata picha ya kalori kwenye vyakula unavyokula mara kwa mara. Hata kama hutaki kuendelea kufuatilia kila siku, zoezi hili litakupa ufahamu mkubwa.
- Jifunze ukubwa wa portions. Gramu 100 za nyama ni kiasi gani? Kikombe kimoja cha wali kina kalori ngapi?
Kama Hutaki Kabisa Kufuatilia Kalori:
Tumia kanuni ya mkufunzi Magnus Lygdbäck (mkufunzi wa Chris Hemsworth – Thor): Kanuni ya 80/20.
- Asilimia 80 ya Milo Yako: Iwe safi, yenye afya, na kiasi sahihi. Fikiria:
- Protini (kuku, samaki, mayai, maharage) kiasi cha kiganja kimoja.
- Mbogamboga zenye nyuzinyuzi nyingi (broccoli, spinach, mchicha) kiasi cha viganja viwili.
- Wanga unaoyeyuka taratibu (viazi vitamu, mihogo, mchele wa brown, quinoa) kiasi cha kiganja kimoja. Hapa tunazungumzia mlo kamili.
- Asilimia 15 Iliyobaki: Hii ni nafasi yako ya kufurahia maisha. Pata kinywaji chako, kipande cha keki, au chakula unachokipenda bila kujilaumu. Hii ndiyo faida za mlo kamili – inakupa nafasi ya kula vizuri mara nyingi na kujiburudisha kidogo.
Kuchagua vyakula vya kupunguza mafuta mwilini mara nyingi (asilimia 80) ndio msingi. Kufahamu unachokula, iwe kwa kufuatilia kalori au kwa kanuni ya 85/15, ni hatua muhimu sana.
Tabia #5: PROTINI KWANZA! Ifanye Mfalme wa Kila Mlo Wako.
Hii ni kanuni ya dhahabu, hasa kwetu sisi wanaume 40+. Huwezi kujenga au kudumisha misuli bila matofali yake – na matofali hayo ni PROTINI.
Umuhimu wa Protini Baada ya 40:
- Kujenga na Kutunza Misuli: Kama tulivyoona, tunapoteza misuli kadri umri unavyosonga. Kula protini ya kutosha ndio njia ya kupambana na hili na kuweka mwili imara. Hii ni sehemu ya mazoezi ya kuongeza mwili kwa mwanaume – kula vizuri.
- Inashibisha Sana: Protini inachukua muda mrefu kumeng’enywa na inakufanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu. Hii inapunguza sana uwezekano wa kula ovyo kati ya milo au kula kupita kiasi kwenye mlo unaofuata. Ni silaha kubwa katika kupunguza mafuta mwilini.
- Inaongeza Uchomaji Kalori (Thermic Effect): Mwili unatumia nishati zaidi kumeng’enya protini ukilinganisha na wanga au mafuta. Kwa hiyo, kula protini zaidi kunaweza kuongeza kidogo metabolism yako.
- Muhimu kwa Homoni na Enzymes: Protini inahusika katika utengenezaji wa homoni muhimu (kama testosterone) na enzymes zinazoendesha michakato mingi mwilini.
Kiasi Gani cha Protini Unahitaji?
Shirika la Afya Duniani (WHO) linapendekeza kama gramu 0.8 kwa kila kilo ya uzito wako. LAKINI, kwa watu wanaofanya mazoezi (na kama uko 40+, unapaswa kuwa unafanya mazoezi!), wataalamu wengi wanapendekeza kiwango kikubwa zaidi: kati ya gramu 1.6 hadi 2.2 kwa kila kilo ya uzito wako.
- Mfano: Kama una uzito wa kilo 80, unahitaji kati ya gramu 128 (80 x 1.6) na gramu 176 (80 x 2.2) za protini kwa siku.
Gawanya Kwenye Kila Mlo:
Badala ya kujaribu kula protini yote kwenye mlo mmoja, ni bora kuigawanya kwenye milo yako yote (mfano: kifungua kinywa, chakula cha mchana, chakula cha jioni). Hii inahakikisha mwili wako unapata ugavi endelevu wa amino acids (vijenzi vya protini) kwa ajili ya kujenga na kukarabati misuli siku nzima.
Fanya Protini iwe Nyota wa Kila Sahani:
Hii ndio nimekuwa nikifanya na imenisaidia sana. Kila ninapoandaa mlo, swali la kwanza najiuliza ni: “Protini yangu iko wapi hapa?”
- Kifungua Kinywa: Badala ya chai na maandazi tu (wanga mtupu), ongeza mayai ya kuchemsha/kukaanga, au weka kipande cha samaki au nyama ya jana iliyobaki. Mtindi wa asili (plain yogurt) au jibini la cottage pia ni vyanzo vizuri.
- Chakula cha Mchana: Hakikisha kuna kipande kizuri cha kuku, samaki, nyama, au sehemu kubwa ya maharage/dengu/choroko.
- Chakula cha Jioni: Kama mchana.
- Snacks (kama unahitaji): Chagua zenye protini – karanga chache, mayai ya kuchemsha, kipande cha jibini.
Mifano Mingine ya Kuongeza Protini:
- Kwenye Wali/Ugali: Ongeza maharage, dengu, au mchuzi wenye nyama/samaki/kuku wa kutosha.
- Kwenye Mboga za Majani: Changanya na karanga zilizosagwa kidogo au mbegu (mf. za maboga).
- Pasta: Chagua zile zilizotengenezwa kwa kunde (dengu nyekundu, choroko) zina protini nyingi zaidi. Changanya jibini.
- Smoothies: Ongeza unga wa protini (protein powder) kama unatumia, au mtindi mzito, au siagi ya karanga.
Kuweka kipaumbele kwenye protini ni moja ya kanuni za afya bora muhimu zaidi utakayojifunza. Itakusaidia kujenga mwili imara, kudhibiti njaa, na kufanya safari yako ya kupunguza mafuta mwilini iwe rahisi zaidi.
Tabia #6: KILA MLO = KOMBO YA KUDHIBITI NJAA (The Hunger Crushing Combo – HCC)
Hapa kuna siri nyingine kubwa ambayo mtaalamu wangu wa lishe alinifundisha, na imebadilisha kabisa jinsi ninavyokula na kudhibiti tamaa za ajabuajabu, hasa ile ya sukari.
Tamaa ya sukari ilikuwa adui yangu mkubwa. Nilikuwa naweza kuacha kula chakula halisi ili nipate nafasi ya kula kitu kitamu chenye sukari. Nilijidanganya kuwa naepuka kalori nyingi (kosa kubwa!).
Tatizo la Sukari na Wanga:
Unapokula sukari au wanga (mkate mweupe, maandazi, soda, pipi), sukari yako kwenye damu inapanda haraka sana (unapata nguvu za ghafla). Lakini, muda mfupi baadaye, inashuka GHAFLA na kuwa chini sana. Hii ndio inakufanya ujisikie mchovu, mwenye njaa tena, na mwenye TAMAA KUBWA ya kula sukari zaidi ili mwili upate nguvu tena. Ni mzunguko mbaya sana (vicious cycle) unaofanya kupunguza mafuta mwilini kuwa kugumu mno. Madhara ya mafuta mwilini yanachochewa na mzunguko huu.
Suluhisho: The Hunger Crushing Combo (HCC)
Mtaalamu wa lishe Abbey Sharp anaita hii “Hunger Crushing Combo”. Ni rahisi: Hakikisha kila mlo wako (na hata snacks zako kama unakula) una mchanganyiko wa vitu vitatu muhimu:
- Protini (P): (Tumekwisha iongelea) Inashibisha na kujenga misuli.
- Mafuta Yenye Afya (F): (Avocado, karanga, mbegu, mafuta ya zeituni, samaki wenye mafuta) Yanashibisha, yanasaidia kunyonya vitamini, na ni muhimu kwa homoni. Usiogope mafuta yenye afya!
- Nyuzinyuzi (Fiber) (F): (Mbogamboga, matunda, nafaka zisizokobolewa, kunde) Zinashibisha, zinasaidia mmeng’enyo wa chakula, na zinapunguza kasi ya sukari kuingia kwenye damu.
Jinsi HCC Inavyofanya Kazi:
Kula hivi vitu vitatu pamoja kunasaidia KUTULIZA kiwango chako cha sukari kwenye damu. Hakuna tena kupanda na kushuka kwa kasi. Hii inapunguza sana tamaa za ajabuajabu (hasa ya sukari) na kukufanya ujisikie umeshiba na mwenye nguvu kwa muda mrefu zaidi. Huu ni msingi wa mlo kamili.
Badala ya Kufanya Hivi… Fanya Hivi:
- Badala ya: Kula biskuti au maandazi peke yake kama kifungua kinywa… Fanya Hivi: Kula mayai (P) na kipande cha parachichi (F) kwenye mkate wa brown (Fibre), au mtindi wa asili (P&F) na matunda (Fibre) na karanga kidogo (F).
- Badala ya: Kula ndizi peke yake kama snack… Fanya Hivi: Kula ndizi (Fibre) pamoja na karanga chache (F&P) au kijiko cha siagi ya karanga (F&P).
- Badala ya: Kula wali na mchuzi mwepesi tu… Fanya Hivi: Hakikisha kuna protini ya kutosha (samaki/kuku/maharage – P), mbogamboga nyingi (Fibre), na labda ongeza parachichi pembeni (F).
- Badala ya: Kula keki peke yake kwa dessert… Fanya Hivi: Kula mlo wako mkuu kwanza (wenye P, F, Fibre), halafu ndipo upate kipande chako kidogo cha keki. Uwezekano ni kwamba hutahitaji kula kikubwa kama ungeanzia na keki.
Kudhibiti sukari kwenye damu ni muhimu zaidi kadri umri unavyosonga ili kuzuia kisukari aina ya 2 na kudhibiti uzito. Kutumia kanuni ya HCC katika kila mlo ni njia bora ya kufanikisha hili, kubaki na nguvu siku nzima, na kupunguza ule “uchovu wa saa nane mchana”. Hii ni sehemu muhimu ya kuelewa afya ya mwili ni nini na jinsi inavyofanya kazi.
Fikiria kila sahani yako kama timu: Protini ni nahodha, Mafuta yenye afya ni kiungo mchezeshaji, na nyuzinyuzi ni mlinzi imara. Timu hii ikikamilika, utashinda vita dhidi ya njaa na tamaa zisizo na maana.
Tabia #7: FURAHIA “KITINDAMLO CHA KIJANJA” Kila Siku (Smart Desserts)
Mimi binafsi napenda vitu vitamu. Kuacha kabisa ilikuwa sio kazi rahisi. Moja ya sheria nilizojiwekea nilipoanza safari hii ni kwamba lazima iwe ENDELEVU na yenye KUFURAHISHA. Maisha mapya hayapaswi kuwa mateso.
Kwa bahati nzuri, mtaalamu wangu wa lishe alikubaliana nami. Alisema ni bora kushirikiana na mwili wako kuliko kupambana nao. Kuruhusu kitindamlo kidogo mara kwa mara ni bora kuliko kujibana sana halafu siku moja ukajikuta unakula boksi zima la biskuti.
Sharti ni Moja Tu: Kitindamlo kiwe cha “KIJANJA”.
“Kijanja” haimaanishi lazima iwe tunda au mtindi tu (ingawa hivyo ni vizuri sana). Kitindamlo cha Kijanja ni kile ambacho:
- Kinakidhi Tamaa Yako: Kinakupa ile raha ya kitu kitamu unayoitafuta.
- HAKIKUSABABISHI KULA KUPITA KIASI: Unakipenda, lakini sio kwa level ya kukufanya upoteze kontrolli na kula kingi mno.
Mfano Wangu wa Kitindamlo cha Kijanja:
- Sorbet ya Limao (Lemon Sorbet): Ile ladha yake ya uchachu-lakini-tamu inanifurahisha, lakini baada ya vijiko vichache tu najisikia nimetosheka. Hainipi ile hamu ya kuendelea kula bila kikomo.
- Chokoleti Nyeusi (Dark Chocolate – 70% Cocoa au zaidi): Chokoleti ya maziwa inanichanganya kabisa, udhibiti unapotea. Lakini chokoleti nyeusi, hasa nikila na kikombe cha chai ya mnanaa (mint tea), inanipa utulivu na raha. Uchungu wake kidogo unanizuia kula kipande kikubwa.
Tafuta Kitindamlo Chako cha Kijanja:
Inaweza kuwa ni matunda fulani unayoyapenda sana (lakini sio yale matamu mno kama embe peke yake), mtindi wenye matunda kidogo, kipande kidogo cha keki unayoipenda lakini sio sana, au hata kinywaji kama kahawa nzuri. Jaribu vitu tofauti uone kipi kinakupa raha bila kukutoa kwenye mstari.
Jambo Muhimu: Bado nakula vile vitindamlo “hatari” (keki) lakini najitahidi iwe mara moja au mbili tu kwa wiki, na kwa kiasi kidogo. Na kwa sababu nimezoea kula vitindamlo vyangu vya “kijanja” kila siku, hata nikikutana na vile “hatari”, ile tamaa kali ya zamani imepungua sana.
Kudhibiti sukari bado ni muhimu. Lakini pia, kujinyima kabisa kunaweza kuleta stress na kukufanya uache mpango mzima. Kuwa na mkakati wa “kitindamlo cha kijanja” kunaleta usawa – unapata raha kidogo bila kuharibu juhudi zako za kupunguza mafuta mwilini na kutunza afya njema.
Tabia #8: ACHA MUDA KATI YA MILO (Give Your Gut a Break!)
Hii ni tabia nyingine ndogo lakini yenye nguvu kubwa kwa afya bora, hasa afya ya utumbo wako. Kujipa muda wa kutosha kati ya milo (angalau saa 3 hadi 4) kuna faida kuu mbili:
- Kuzuia Kula Kila Wakati (Grazing): Kula vitu vidogovidogo kila mara, hata kama ni vyenye afya, kunaongeza kalori zako bila wewe kujua. Kila kalori inahesabika. Kuweka nafasi kati ya milo kunasaidia kudhibiti jumla ya kalori unazokula kwa siku.
- Kuamsha Mfumo wa Usafi Tumboni (Migrating Motor Complex – MMC): Hapa kuna kitu cha kitaalamu kidogo lakini muhimu. Kuna mfumo ndani ya utumbo mdogo wako unaoitwa MMC. Huu mfumo unafanya kazi kama “wafagiaji” – unasafiri kwenye utumbo na kusukuma mabaki ya chakula, bakteria, na uchafu mwingine kuelekea kwenye utumbo mkubwa. LAKINI, huu mfumo unaamka na kufanya kazi vizuri tu pale ambapo HUJALA kwa muda fulani (kama saa 2 hadi 4 hivi). Ukiwa unakula kila wakati, unazuia MMC kufanya kazi yake vizuri. Hii inaweza kuchangia matatizo kama gesi, kujaa tumbo, na hata ukuaji wa bakteria wabaya kwenye utumbo mdogo (SIBO).
Changamoto na Suluhisho:
Mwanzoni, kuzoea hii tabia inaweza kuwa ngumu. Ile njaa ndogo inaweza kukutembelea kati ya milo.
Kilichonisaidia mimi (na kinaweza kukusaidia wewe) ni hiki:
- Hakikisha Milo Mikuu Unashiba VIZURI (Lakini Siyo Kuvimbiwa): Hapa ndipo ile Kanuni ya HCC (Protini + Mafuta yenye Afya + Nyuzinyuzi) inapoingia tena. Ukila mlo kamili unaoshibisha vizuri, hutapata njaa haraka kati ya milo. Kifungua kinywa imara kitakufikisha vizuri hadi chakula cha mchana. Chakula cha mchana imara kitakufikisha hadi cha jioni.
Afya ya utumbo inahusiana sana na afya ya mwili mzima, ikiwemo kinga ya mwili, mood, na hata uzito. Kuupa utumbo wako mapumziko kati ya milo kwa kuacha kula kila wakati ni njia rahisi ya kuboresha afya ya utumbo wako na kusaidia mwili kufanya kazi vizuri zaidi. Hii ni sehemu ya kanuni za afya bora ambazo mara nyingi hazizingatiwi.
Jaribu kuweka gap la angalau saa 3 kati ya kifungua kinywa na chakula cha mchana, na saa 4 kati ya chakula cha mchana na cha jioni. Kunywa maji mengi kati ya milo kama unajisikia njaa kidogo.
Tabia #9: UKITOKA AU UKISAFIRI, MBOGA KWANZA! (Prioritize Veggies When Eating Out)
Tunajua inavyokuwa. Umetoka na washkaji, mko safarini, au mmealikwa sehemu. Kufuatilia kalori au kufuatilia sana diet inakuwa ngumu na inachosha. Unataka kurelax na kufurahia.
Na ni sawa kabisa! Afya bora haimaanishi kujinyima kila kitu na kutengwa na jamii.
LAKINI…
Kujiachia sana kila ukitoka kunaweza kurudisha nyuma juhudi zako zote za kupunguza mafuta mwilini. Unaweza kurudi kutoka safarini au weekend ukiwa umeongeza kilo kadhaa na kujisikia vibaya.
Sheria Yangu Rahisi Ninapotoka/Kusafiri:
Ni rahisi sana: MBOGA KWANZA!
Mbali na kuhakikisha napata protini yangu na mlo unakaribia kuwa HCC (hizi zimekuwa tabia sasa), najitahidi KULA MBOGAMBOGA NYINGI kwanza, kabla ya kitu kingine chochote kwenye sahani.
- Mfano: Jumamosi iliyopita tulikwenda sehemu ya pizza na marafiki. Zamani, ningeagiza pizza yangu na kuila yote. Sasa, mimi na mshikaji wangu tulishare kwanza SALADI KUBWA ya kuku, halafu ndio tukashare pizza. Matokeo? Nilishiba nikiwa nimekula kama NUSU tu ya kiasi cha pizza nilichokuwa nakula zamani.
- Kwenye Buffet: Anza na kujaza sahani yako na aina mbalimbali za saladi na mbogamboga zilizopikwa (zisizo na mafuta mengi au sosi nzito). Baada ya hapo, ndio uchukue protini (nyama/samaki/kuku) na kiasi kidogo cha wanga (wali/viazi).
- Kwenye Mkahawa: Agiza side dish ya mboga za majani au saladi pamoja na mlo wako mkuu. Anza kula hizo kwanza.
Faida za Mbinu Hii:
- Unashiba Haraka na Kalori Chache: Mbogamboga zina nyuzinyuzi (fiber) na maji mengi, zinajaza tumbo haraka bila kalori nyingi. Hii inakuacha ukiwa na nafasi ndogo ya kula vyakula vingine vyenye kalori nyingi zaidi.
- Unapata Virutubisho Muhimu: Mbogamboga zimejaa vitamini, madini, na antioxidants ambazo ni muhimu kwa afya njema.
- Inasaidia Mmeng’enyo: Fiber kwenye mboga inasaidia kuzuia kuvimbiwa (constipation), jambo ambalo linaweza kuwa tatizo hasa unaposafiri au kubadilisha mazingira ya chakula. Faida mbili kwa moja!
Hii ni njia rahisi na “kijanja” ya kufurahia kutoka bila kuharibu kabisa mpango wako wa afya bora.
Tabia #10: ENDELEA KUJIFUNZA NA KUJIKUMBUSHA FAIDA (Stay Educated & Motivated)
Hii inaweza kuonekana kama sio tabia ya moja kwa moja ya kula au kufanya mazoezi, lakini kwangu mimi, imekuwa na nguvu kubwa sana ya KUNIFANYA NIENDELEE.
Ukweli ni Huu: Hamasa inapanda na kushuka. Kutakuwa na siku utaamka hujisikii kabisa kwenda gym au kuchagua chakula kizuri. Hapo ndipo hii tabia inapoingia.
Ninachofanya:
- Nikihisi Uvivu wa Mazoezi: Najikumbusha kwa kusoma makala au kuangalia video fupi kuhusu umuhimu wa mazoezi kwa afya ya moyo, ubongo, kudhibiti uzito, kuongeza testosterone, na kuishi maisha marefu yenye ubora. Kukumbuka “KWANINI” nafanya mazoezi kunanipa nguvu mpya ya kuinuka na kwenda. Mazoezi ni afya, na kujikumbusha hili mara kwa mara ni muhimu.
- Nikiwa Karibu Kula Hovyo: Najikumbusha jinsi chakula kinavyoathiri mwili wangu – sio tu uzito, bali nguvu zangu, mood yangu, afya yangu ya muda mrefu, na hata “performance” yangu. Kuangalia video kuhusu faida za mlo kamili au kusoma kuhusu madhara ya sukari nyingi kunanisaidia kutulia na kufanya chaguo bora zaidi. Ninaukumbuka mwili wangu wa sasa na wa baadaye.
- Nikila Kitu Kizuri Kiafya: Najitahidi kujua faida zake. Kwa mfano, nikila parachichi, najikumbusha kuhusu mafuta yake mazuri kwa moyo na ubongo. Nikila mchicha, nawaza kuhusu iron na vitamini K. Hii inafanya uzoefu wa kula kiafya kuwa wa kufurahisha zaidi – najisikia vizuri kwa kuutunza mwili wangu.
Jinsi Unavyoweza Kuanza:
- Tumia Google kutafuta “faida za kuwa na afya bora” au “umuhimu wa afya bora”. Soma makala chache.
- Tembelea mara kwa mara jukwaa letu la Recharge My40 Brotherhoo. Nitaliongelea kwa urefu hapa chini.
- Fuatilia kurasa au chaneli za YouTube/Podcast zinazozungumzia afya kwa njia inayoeleweka na kukupa motisha (kama ile ya Huberman Lab niliyoitaja, ingawa iko kwa Kiingereza, tafuta hata za Kiswahili zenye maudhui mazuri).
- Unapokula chakula cha afya, chukua dakika moja kufikiria jinsi kinavyousaidia mwili wako.
Kujielimisha na kujikumbusha faida za mtindo huu wa maisha kutakupa motisha endelevu itakayokusaidia kuvuka zile siku ngumu na kubaki kwenye njia sahihi ya afya bora.
Sasa, Hebu Tuunganishe Yote Pamoja… na Nikupe Siri Kubwa Zaidi
Umeona hizi tabia 10. Ni nzuri, zinafanya kazi, na zimenisaidia mimi (na wengine wengi) kufikia na kudumisha umbo zuri na kupunguza mafuta mwilini. Ni msingi imara wa afya bora.
LAKINI, bro, Ukweli ni Huu: Kwa sisi wanaume tuliofika 40+, kuna zaidi ya haya tu. Kuna mambo yanayoendelea “chini ya hood” ambayo haya mazoea pekee hayawezi kuyatatua kikamilifu.
Hizi tabia 10 ni kama kujenga nyumba nzuri kwa nje. Inaweza kupendeza, lakini kama msingi wake (foundation) ni mbovu, nyumba hiyo haitadumu na itakuwa na matatizo mengi ya ndani.
Msingi wa Uanaume Wako Baada ya 40 Uko Wapi?
Kwa mwanaume anayejali afya yake kwa ukamilifu baada ya miaka 40, kuna maeneo mawili muhimu sana ambayo yanahitaji uangalizi wa kipekee, maeneo ambayo ndio MSINGI wa nguvu na uhai wake kama mwanaume:
- AFYA YA TEZI DUME (PROSTATE HEALTH): Hili ni kiungo kidogo lakini muhimu sana. Kadri umri unavyosonga, tezi dume linaweza kutanuka (BPH) na kusababisha shida za kukojoa, au hata kupata matatizo makubwa zaidi. Afya ya tezi dume lako inaathiri moja kwa moja mfumo wako wa mkojo na hata afya yako ya tendo la ndoa.
- NGUVU ZA KIUME NA UTENDAJI (SEXUAL PERFORMANCE & VITALITY): Hili ni eneo ambalo linaathiriwa moja kwa moja na mabadiliko ya homoni (testosterone), mtiririko wa damu, afya ya mishipa, stress, na hata afya ya tezi dume. Kupunguza mafuta mwilini kunaweza kusaidia, lakini sio suluhisho lote.
Hapa ndipo wengi wetu tunakwama. Tunahangaika na mazoezi na diet za jumla, lakini tunasahau kushughulikia MSINGI. Unakuta mtu ana mwili mzuri kwa nje, lakini ndani bado anasuasua, tezi dume inaleta shida, na “performance” chumbani sio ile anayoitamani.
Ndio Maana Tukaamua Kufanya Kitu Zaidi…
Baada ya kupitia haya mwenyewe, kujifunza kwa kina, na kuona matokeo chanya kwangu, nilitambua kuwa kuna haja ya kutoa MWONGOZO MAALUM kwa wanaume wenzangu wa 40+. Mwongozo ambao hauishii tu kwenye kupunguza mafuta mwilini, bali unazama kwenye kiini cha changamoto zetu – AFYA YA TEZI DUME na KURUDISHA NGUVU ZA KIUME zile za ujana.
Nimekusanya maarifa yote muhimu, siri ambazo madaktari wengi hawana muda wa kukuelezea, na mikakati ya LISHE na MTINDO WA MAISHA iliyothibitishwa kisayansi na kimapokeo kusaidia maeneo haya mawili muhimu.
Na nimeyaweka yote kwenye KITABU KIMOJA cha kipekee kilichoandikwa kwa lugha rahisi, Kiswahili kitamu unachokielewa.
Ninakuletea…
Hiki sio kitabu cha kawaida cha “jinsi ya kupunguza uzito”. HAPANA! Hiki ni kitabu kinachozama moja kwa moja kwenye yale yanayotusumbua SISI WANAUME 40+:
- Utajifunza kwa KINA kuhusu Tezi Dume lako: Jinsi linavyofanya kazi, kwanini linabadilika baada ya 40, dalili za hatari za kuzingatia, na muhimu zaidi, NJIA ASILIA za kulilinda na kuliweka katika afya njema bila kutegemea dawa zenye madhara.
- Utagundua SIRI za Kurudisha na Kuongeza Nguvu za Kiume MARA MBILI (2x Performance): Tutachambua sababu za kisayansi za kupungua kwa nguvu (homoni, mzunguko wa damu, stress, lishe duni) na kukupa MIKAKATI MAALUM ya lishe, virutubisho muhimu (vilivyofichwa ambavyo huambiwi), na mazoezi mepesi ya kuongeza mtiririko wa damu na homoni zako kiasili. Utajifunza jinsi ya kumfanya mpenzi wako ASHANGAE na kuomba zaidi!
- Utapata Mpango Rahisi wa Lishe kwa Mwanaume 40+: Sio diet kali, bali mwongozo wa vyakula gani uongeze na vipi upunguze ili kuimarisha tezi dume, kuongeza testosterone, na kuboresha afya ya moyo na mishipa (muhimu kwa “performance”). Utajua mlo kamili ni nini hasa kwa mahitaji yako sasa.
- Na Mengi Zaidi…
Hiki kitabu ni kama kuwa na mtaalamu rafiki yako anayekushika mkono na kukuongoza kwenye njia sahihi ya kurudisha UJANA na NGUVU zako baada ya 40.
Lakini Subiri, Kuna Zaidi… Hapa Ndipo “BROTHERHOOD” Inapoingia!
Najua safari hii ya afya bora inaweza kuwa na upweke kidogo. Unajaribu kubadilika, lakini watu wanaokuzunguka hawakuelewi. Unahitaji kuwa na WENZAKO – wanaume wengine kama wewe, wanaopitia changamoto kama zako, wanaoelewa unachojaribu kufanya.
Ndio maana tumeunda kitu MAALUM SANA: The Recharge My40+ BROTHERHOOD!
Hili ni JUKWAA LA SIRI, la wanaume pekee (40+), ambapo tunakutana online (Intranet yetu maalum) kwa ajili ya:
- Kushirikishana Uzoefu: Nini kinafanya kazi, nini hakifanyi kazi.
- Kuuliza Maswali kwa Uhuru (Hakuna Aibu): Hapa ni sehemu salama kuuliza maswali yoyote kuhusu afya, tezi dume, nguvu za kiume, bila kuhukumiwa.
- Kupeana Motisha na Msaada: Tunashikana mkono kwenye safari hii.
- Kupata Maarifa ya Ziada (Advanced Tips): Kuna mambo mengine hatuwezi kuyaweka hadharani, tunashare ndani ya Brotherhood.
- Kujenga Urafiki na Wanaume Wenzako: Connection na watu wenye nia moja.
Brotherhood sio kwa kila mtu. Ni kwa wale ambao wako SERIOUS kuhusu kubadilisha afya zao na kurudisha nguvu zao. Ni kwa wale ambao wamechoka kuwa wanyonge na wanataka kuwa WANAUME KWELI KWELI katika kila Nyanja ya maisha yao.
Sasa, Swali ni Je, Unaingiaje Kwenye Hii Brotherhood ya Kipekee?
Tiketi yako ya kuingia, ufunguo wako wa kufungua mlango wa Brotherhood, ni kitu kimoja tu:
KUNUNUA NA KUSOMA KITABU CHA “Recharge My40+…”
Ndiyo! Kwa bei ndogo tu ya $9 (kama TZS 20,000/=), sio tu unapata kitabu kilichojaa SIRI za kubadilisha maisha yako, bali unapata pia UANACHAMA WA BURE WA MAISHA kwenye jukwaa letu la Brotherhood!
Fikiria: Kwa gharama ya lunch yako moja tu mjini, unapata mwongozo kamili wa kutatua changamoto zako kubwa za kiafya baada ya 40 NA unapata access ya kudumu kwenye community ya wanaume wenzako wenye nia moja. Hii ni ofa ambayo huwezi kuikosa!
Kwanini Tunafanya Hivi?
Tunataka kujenga kwanza UAMINIFU na wewe. Tunataka kukuonyesha THAMANI tunayoweza kukupa kabla hatujaongea mambo makubwa zaidi. Tunajua ukinunua hiki kitabu, ukakisoma, na ukajiunga na Brotherhood, UTAONA MATOKEO. Na hapo ndipo utakuwa tayari kwa hatua inayofuata (ambayo tutaiongelea ndani ya kitabu na Brotherhood – suluhisho letu kamili la “Recharge My40+ Pack“). Lakini kwa sasa, lengo letu ni KUKUPATIA HIKI KITABU na KUKUKARIBISHA KWENYE BROTHERHOOD.
Wakati Unaenda… Nafasi Kwenye Brotherhood Inaweza Kuwa na Kikomo.
Ingawa tunataka kusaidia wanaume wengi iwezekanavyo, ili kudumisha ubora na usiri wa jukwaa letu la Brotherhood, tunaweza kulazimika kuweka kikomo cha idadi ya wanachama wapya tunaowapokea kwa wakati mmoja.
Usisubiri hadi uambiwe “nafasi zimejaa”. Chukua hatua SASA HIVI. Fanya uwekezaji mdogo kwenye afya yako leo, pata maarifa yatakayobadilisha maisha yako, na jiunge na kundi la washindi – The Recharge My40+ Brotherhood.
Hivi Ndivyo Unavyofanya:
- Bonyeza link hii sasa hivi.
- Fanya malipo salama ya $9 (au TZS 20,000).
- Pakua (download) kitabu chako cha eBook papo hapo.
- Ndani ya kitabu (na kwenye email utakayopokea), utapata maelekezo ya jinsi ya kujiunga na Brotherhood.
Ni rahisi hivyo!
Acha kuishi kwa kubahatisha. Acha madhara ya mafuta mwilini yakuandame. Acha dalili za kuzeeka zikutawale. Chukua udhibiti wa afya yako, nguvu zako, na maisha yako kama mwanaume.
Safari yako ya kuwa “Recharged” baada ya 40 inaanzia HAPA, na kitabu hiki ndio RAMANI yako.
Bonyeza Hapa Kupata Kitabu Chako na Kujiunga na Brotherhood SASA!
Nakusubiri ndani ya Brotherhood, Mzee Mwenzangu! Pamoja tutashinda.